Thursday, September 12, 2024

TGNP yatoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa dini Mtwara

 TGNP yawanoa viongozi wa dini,ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi

Na Deogratius Koyanga, Mtwara


 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa viongozi wa dini zote ili waweze kuhamasiaha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi

 Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya mradi wa “mwanamke Ongoza’ unaotekelezwa na TGNP kwa ushirikiano na Taasisi ya Aga khan Foundation kwa  ufadhili wa serikali ya watu wa Canada, yanafanyika wakati nchi yetu ikielekea kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka huu 2024, kukiwa na mkazo kuhusu kushawishi wanawake wajitokeze zaidi kwenye nafasi za uogozi.

 Akiozungumza Mchungaji Michael Namakwana,  wa Kanisa la Bapitist Mtwara alisema kwamba mafunzo ya viongozi wa dini juu ya usawa wa Kijinsia na ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi yatawezesha kuleta mabadiliko makubwa kwasababu baada ya kupata maarifa na uelewa wa masuala ya kijinsia watatumia majukwaa yote ya kanisa kuhakikisha wananachi wanapata elimu  na wanawake wanajitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa na watashinda.

 “sisi viongozi wa dini kwa nafasi zetu tunaalikwa na viongozi wa serikali pia kushiriki mikutano ya vijiji nay a kata, tutatumia nafasi hiyo kuzungumzia masuala haya ili ujumbe ufike kwa mapana yake..” alisema Mchungaji

 Kwa upande wa wasilam, sheikh, Yusuf Salum Mwandewa, kutoka kata ya Mkunwa alisema kwamba viongozi wa vyma vya siasa wajitahidi kutoa nafasi kwa wanawake wanaotarajia kugombea nafasi badala ya kuwarudisha nyuma au kuwalazimisha kugombea viti maalum.

 Mwenyekiti wa Kanisa Katoliki Kigango cha Dihimba,Jimbo Katoliki la Mtwara,  Selestine Lukanga alisema kwamba wao watatumia majukwaa yote ya ndani ya kanisa kuanzia ngazi ya Kigango, hadi jumuiya ndogondogo, hasa wakati wa matangazo kanisani na kuvitembelea vyama vya kitume vyote kuwapa elimu ya masuala ya kijinsia, ikiwepo kuweka mikakati ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto.

 













 

 

 


No comments:

Post a Comment