Friday, September 20, 2024

WaterAid, TGNP na TAWASANET wajenga uwezo kwa wanawake Hanang’

 WaterAid, TGNP na TAWASANET wajenga uwezo kwa wanawake Hanang’


Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya wanawake viongozi wa Halmashauri za vijiji na kamati mbalimbali wilayani Hanang' Mkoa wa Manyara


Na Deogratius Koyanga, Manyara

Taasisi ya WaterAid Tanzania,  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), na Mtandao wa Asasi za Kiraia zinazoshughulikia Maji, na Usafi wa Mazingira Tanzania (TAWASANET), wamefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wanawake viongozi kutoka vijiji nane (8) katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara.

Mafunzo hayo yanalenga kujenga uwezo kwa viongozi wanawake wanaohudumu kwenye Kamati za zahanati na Vituo vya afya, shule za msingi, Bodi za Sekondari na kamati za Huduma za jamii kwenye Halmashauri za vijiji ili waweze kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa rasilimali ili kutatua changamoto za maji na Usafi wa mazingira (WASH) katika maeneo yao.

WaterAid, TGNP na TAWASANET  wanatekeleza kampeni ya Afya ya Mwanamke Sasa ambayo inalenga kujenga uwezo kwa wanawake na wanaume ili kuondoa changamoto za Kijinsia kwa kuzipa kipaumbele wakati wa mipango na bajeti sambamba na kuondoa changamoto za kijinsia ambazo zina wakabili zaidi wanawake.

Akiungungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Ushawishi,  na Uchechemuzi wa sera kutoka WaterAid, Christina Mhando, alisema kwamba suala la ukosefu wa maji ni suala la wanawake, na ni suala la kijinsia, kwahiyo wanawake wanapaswa kulipa kipaumbele katika majadiliano, au maamuzi ya kupanga vipaumbele vya bajeti. “ …. Hata yanapoibuka magonjwa, waathirika wakubwa ni wanawake ndio maana tunashirikiana na wenzetu hawa kujenga uelewa wa jamii  jinsi ambavyo masuala ya maji, afya na usafi wa mazingira unavyoweza kuathiri wanawake, watoto wa kike na wazee  sambamba kurasimisha masuala ya kijinsia katika sera, bajeti na mipango yote ya serikali za Mitaa” alisema Mhando.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang, Theresia Irafy, wakati wa kufungua mafunzo hayo alisema kwamba, mafunzo hayo ni muhimu kwa wakati huu ukizingatia kwamba wanawake ndio wahitaji  na watumiaji wakubwa wa huduma za maji na endapo watapata uelewa na kusimamia vizuri rasilimali za umma sambamba na miradi iliyojengwa italeta tija na kuwezesha kumtua mwanamke ndoo kichwani.

“Ninashukuru wadau hawa kwa kuja Hanang, tunahitaji sana wadau wanaofanya kazi ya kujenga uelewa kwa jamii na kubadilisha mitazamo hasi kuhusu masuala ya kijinsia, mtawezesha kubadilisha mitazamo ya jamii, lakini pia wanawake wanatakiwa kuwa viongozi wazuri wa kusimamia miradi hii sambamba na kuibua  na kuweka vipaumbele vya bajeti vyenye mtazamo wa kijinsia” alisema

Mafunzo hayo pia, yamefungwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Bi. Rose Kamili ambaye alisema kwamba  suala la maji na usafi wa mazingira ni suala la kijinsia na linatakiwa kuwekewa mkazo kwa wanawake kulielewa na kulisimamia wenyewe kwasababu  ndio kundi linaloathirika zaidi endapo huduma za maji na usafi wa mazingira zitakosekana.

“Sisi Halmashauri, tunaendelea kupambana kuhakikisha tunatatua changamoto za ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo, lakini tuendelee kuwashukuru wadau wetu WaterAid kwa kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa baadhi ya vijiji hasa kwenye taasisi kama zahanati ambako wanawake wanapata huduma zaidi. WaterAid mmekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wa Hanang, tunawashukuru sana…” alisema Kamili.

Mafunzo hayo yamewahusisha wanawake kutoka vijiji nane ambavyo ni Gidamula, Gawidu, Muungano, Dajameda, Laghanga,  Wareta, Getak na Bashang, ambapo  washiriki wamekubaliana kuhakikisha wanahamasisha wanawake kujitokeza kugombea uongozi katika serikali za Mitaa mwaka huu 2024 ili waweze kuwa kwenye nafasi za maamuzi hasa kuibua miradi ya maendeleo itakayotatua changamoto za Maji, afya na usafi wa mazingira (WASH) katika jamii.












Picha ya pamoja kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Mhe. Rose Kamili na wawezeshaji kutoka TGNP, TAWSANET na WaterAid, baada ya kufunga mafunzo ya wanawake viongozi mjini Hanang'

 

Thursday, September 12, 2024

TGNP Empowers Religious Leaders to Champion Women's Leadership

 TGNP Empowers Religious Leaders to Champion Women's Leadership



By Deogratius Koyanga, Mtwara

The Tanzania Gender Network (TGNP) has conducted training programs for religious leaders to empower them to advocate for women's leadership and gender  equality.

As part of the "She Leads" or “mwanamke Ongoza” project, these trainings aim to break down barriers that have traditionally limited women's participation in politics. The project is a joint effort by TGNP and the Aga Khan Foundation, supported by the Canadian government.

With Tanzania's upcoming local government elections, these trainings are particularly timely. They seek to inspire more women to run for office and create a more inclusive political landscape.

Pastor Michael Namakwana of the Mtwara Baptist Church highlighted the crucial role of religious leaders in promoting gender equality. He emphasized the need for these leaders to educate their communities and encourage women to participate in the political process.

Sheikh Yusuf Salum Mwandewa, a Muslim leader from Mkunwa ward, called on political parties to ensure equal opportunities for women candidates. He urged them to avoid discouraging women from running for office or forcing them into special seats positions.

Celestine Lukanga, chairman of the Catholic Church's Dihimba outstations - Mkunwa Parish, stated that the church will actively promote gender equality and combat gender-based violence. They will educate their members and develop strategies to protect women and children.

Through these training programs, TGNP is working to equip religious leaders with the knowledge and tools to become powerful advocates for women's rights. By empowering these leaders, TGNP aims to create a more inclusive and equitable society.
















TGNP yatoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa dini Mtwara

 TGNP yawanoa viongozi wa dini,ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi

Na Deogratius Koyanga, Mtwara


 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa viongozi wa dini zote ili waweze kuhamasiaha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi

 Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya mradi wa “mwanamke Ongoza’ unaotekelezwa na TGNP kwa ushirikiano na Taasisi ya Aga khan Foundation kwa  ufadhili wa serikali ya watu wa Canada, yanafanyika wakati nchi yetu ikielekea kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka huu 2024, kukiwa na mkazo kuhusu kushawishi wanawake wajitokeze zaidi kwenye nafasi za uogozi.

 Akiozungumza Mchungaji Michael Namakwana,  wa Kanisa la Bapitist Mtwara alisema kwamba mafunzo ya viongozi wa dini juu ya usawa wa Kijinsia na ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi yatawezesha kuleta mabadiliko makubwa kwasababu baada ya kupata maarifa na uelewa wa masuala ya kijinsia watatumia majukwaa yote ya kanisa kuhakikisha wananachi wanapata elimu  na wanawake wanajitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa na watashinda.

 “sisi viongozi wa dini kwa nafasi zetu tunaalikwa na viongozi wa serikali pia kushiriki mikutano ya vijiji nay a kata, tutatumia nafasi hiyo kuzungumzia masuala haya ili ujumbe ufike kwa mapana yake..” alisema Mchungaji

 Kwa upande wa wasilam, sheikh, Yusuf Salum Mwandewa, kutoka kata ya Mkunwa alisema kwamba viongozi wa vyma vya siasa wajitahidi kutoa nafasi kwa wanawake wanaotarajia kugombea nafasi badala ya kuwarudisha nyuma au kuwalazimisha kugombea viti maalum.

 Mwenyekiti wa Kanisa Katoliki Kigango cha Dihimba,Jimbo Katoliki la Mtwara,  Selestine Lukanga alisema kwamba wao watatumia majukwaa yote ya ndani ya kanisa kuanzia ngazi ya Kigango, hadi jumuiya ndogondogo, hasa wakati wa matangazo kanisani na kuvitembelea vyama vya kitume vyote kuwapa elimu ya masuala ya kijinsia, ikiwepo kuweka mikakati ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake na watoto.