Thursday, September 28, 2023

TGNP yaendesha Mjadala wa 'Nafasi Salama' kwa wenza wa viongozi wanawake

 

 

Na Mwandishi wetu, Kondoa

Mtandao wa Kijinsia Nchini (TGNP) kwa kushirikiana na Mfuko wa Aghakan(AKF-T) kupitia mradi wa ‘’SHE LEADS’’(Mwanamke Ongoza) kwenye Halmashauri ya Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma, imeendesha Mjadala wa nafasi salama ‘safe space’ na baadhi ya Wanaume wenza wa Viongozi wanawake wanaotoka katika vitongoji na vijiji vya kata ya Haubi .








Akiongoza mjandala huo mwezehaji kutoka TGNP, Deogratius Temba, amesema lengo la mjadala huo ni kubadilisha Mtazamo,Mila na Desturi hasi kuhusu Ushiriki wa Wanawake kwenye nafasi za Uongozi na kuongeza ushirikiano wa wenza katika kuongeza ufanisi kwa viongozi walioko madarakani.

Ameongeza kuwa kuna kila haja ya wanaume wenye wake viongozi kuwasaidia wake zao  baadhi ya majukumu ambayo yamezoeleka ni ya wanawake hasa ya kijinsia ili kuwapunguzia viongozi wanawake mzigo wa kazi na kuwawezesha kutekeleza majukumu ya kiuongozi kwa manufaa ya Taifa na kuleta tija na heshima kwa viongozi wanawake.

“wanawake wengi, wanakabiliwa na mlundikano wa majukumu mazito ya kifamilia, ambayo yangeweza kufaywa na wanaume au wenza wao. Lakini pia, mtazamo hasi juu ya uwezo wa wanawake kuongoza unaanzia kwenye ngazi ya familia, hii ina athiri kwa kiasi kikubwa utendaji wao, Mila na desturi, misimamo ya kiimani inachochea sana kurudisha nyuma hii hali” alisema Temba.


Wakichangia mjadala baadhi ya Washiriki(wanaume) kupitia Picha chokoziwamesema wanawake viongozi ngazi ya kata,vijiji na vitongoji wanakumbwa na changamoto mbalimbali zinazohusiana na mwingiliano wa majukumu ya Kifamilia pamoja na Uongozi

Wakihitimisha mjadala huo washiriki hao wamesema wanaume wanapaswa kuwa tayari kuwasaidia wake zao majukumu ya nyumbani,kuwapa ushirikiano kupitia mahitaji yao ,kuwajengea uwezo wa kujiamini wanaposhiriki kwenye majukum yao pamoja kuachana na tabia ya mifumo dume.

Kata ya Haubi, ina vijiji Vinne ambavyo ni Haubi, Mwisanga, Mafai na Ntomoko, kati ya hivyo, kijiji cha Haubi pekee chenye vitongoji vinane (8) ndio vina wenyeviti wa vitongoji wanawake watatu (3). Lakini pia, wanawake walioko katika Halmasahuri za vijiji wanakumbana na changamoto kubwa ya kuacha majukumu ya kiuongozi na kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kifamilia kama kutafuta maji na kuhudumia familia.

 

No comments:

Post a Comment