Wednesday, August 30, 2023

TGNP yafanya zoezi la SAM kwa mtazamo wa Kijinsia sekta ya Afya

 

·        *  Watumishi wa afya wanaoishi kwenye wodi ya wazazi kuhamishwa

·       *  Changamoto ya maji kwenye zahanti yaibuliwa

·         *Uongozi wa Vijiji kusimamia vichomea taka zahanati

Na Deogratius Temba, Kondoa

WATUMISHI  wa zahanati ya Kijiji cha Mafai,Kata ya Haubi, Wilaya ya Kondoa  wanaoishi katika wodi zilizojengwa kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto, wametakiwa kutafuta nyumba za kuishi ili kupisha wodi hizo kutumika kwa lengo husika.

Akizungumza wakati wa kujibu hoja zilizoibuliwa kwenye zoezi la Uwajibikaji na Ufuatiliaji wa Jamii (SAM) kwa mtazamo wa Kijinsia, lililoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),  katika sekta ya afya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa,Mashauri Visenti, alisema kwamba watumishi wa zahanti ya Mafai, ambao wanaishi kwenye wodi za Mama na Mtoto wanapaswa kuhamia kwenye nyumba za kupanga kijijini ili kupisha huduma ya mama na mtoto kuendelea katika vyumba hivyo kwa ufanisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama wa vifaa vilivyopo kwenye zahanati hiyo.

Timu ya SAM ikiwa nje ya Jengo la zahanati ya Mafai, ilipotembelea kuona ubora wa utoaji wa huduma za afya

“kwa sababu sasa tumeshatimiza mwaka mmoja tangu kuanza kazi kwa zahanati hii, tunashauri, wapishe zile wodi ili kuboresha Zaidi huduma ya mama na mtoto katika zahanati yetu ile..” alisema Mashauri.

Timu ya SAM ikiendelea na uchambuzi na mapitio ya nyaraka mbalimbali za Halmashauri ya Kondoa DC kwa muda wa siku tatu


Awali akizungumzia jambo hilo, Katibu wa Afya wilaya ya Kondoa, alisema kwamba, awali watumishi hao walikuwa wapya, na ndio walipelekwa kwa ajili ya kuanzisha zahanati hiyo mpya, wakaomba kuishi kwenye vyumba hivyo vya zahanati ili waweze kuzoea mazingira na kutafuta vyumba katika kijiji hicho.

“sasa wamezoea, mazingira, na wameshakaa Zaidi ya mwaka, awali tuliwaruhusu kwa sababu ndio walikuwa wanaenda kuanza kazi katika kijiji kile, tutawa andikia barua ya kuwataka kutafuta nyumba kijijini ili waweze kupisha huduma ziendelee pale. Pia sio salama kiafya kwa wahudumu kuishi ndani ya Hospitali au vyumba vya matibabu.” Alisema Mbaga.

Awali akiwasilisha matokeo ya SAM kwa wadau wa Halmashauri pamoja na Menejimenti, Mwezeshaji wa SAM kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Deogratius Temba alisema kwamba, pamoja na changamoto ambazo zilioonekana za kibajeti, na utoaji wa huduma za afya kwa kuzingatia usawa wa Kijinsia, Halmashauri ya wilaya ya Kondoa imejitahidi kutenga bajeti ya afya kwa mrengo wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kupata hati safi kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/2022.

Mwezeshaji Deogratius Temba, kutoka TGNP akitoa mafunzo mafupi maana ya SAM kwa mrengo wa Kijinsia, umuhimu wake  na maeneo Muhimu ya Kijinsia ya kufuatilia

Temba aliishauri halmasahuri kuweka uzito na umuhimu katika maeneo ambapo kuna vifaa tiba vya mama na mtoto vitumike  na kutunzwa. Mfano, zahanati ya Mafai, wahudumu wanatumia vyumba vya wodi ya mama na mtoto kwa malazi, chumba kinachotumika kwa sasa kama wodi na chumba cha kujifungulia (labor Room) kipo eneo la wazi  karibu na ukumbi wa OPD. Hakuna usiri wala faragha Kwa mama anayejifungua.

“ ..Kutokana na kutokutumika kwa wadi ya mama na mtoto iliyonjengwa kwa kazi hiyo, uhifadhi  na utunzaji wa vifaa tiba na mashine za kisasa zilizonunuliwa kwa ajili  mama na mtoto unakuwa dhaifu.  Mfano mashine nzuri za Oxygen, kuvuta uchafu kwenye pua za watoto wachanga (suction machine) na sterilizer ya kisasa vilikutwa chini kwenye sakafu” alisema temba na Kuongeza:

“ Hatukuona bajeti  kwa ajili ya Zahanati ili kuhakikisha zinapata maji safi na salama kwa ajii ya mahitaji ya kina mama wanaojifungua. Hata tulipoitembelea Zahanati ya Mafai kisima kilichopo jirani hakijaanza kutumika, lakini pia kina mama wanaojifungulia zahanati hawana huduma ya maji….” Alisema Temba

Aidha timu ya SAM kwa mrengo wa Kijinsia iliishauri Halmashauri kutenga  bajeti kwa ajili ya nyumba za watumishi kwani kuna maboma ya nyumba za watumishi wa kada ya afya ambazo zimejengwa na jamii kwa nguvu zao, lakini zipo hatua ya lenta muda mrefu. Mwaka wa fedha 2021/2022 hakuna bajeti iliyotengwa kwa ajili ya nyumba za watumishi wa afya huko vijijini, Mfano jengo  nyumba ya watumishi Zahanati ya Mafai ambalo limejengwa na wananchi hadi hatua ya lenta tangu mwaka 2014, sasa limeanza kuharibika.

Zoezi la SAM na mafunzo yake liliendeshwa kwa njia shirikishi za kiraghibishi ili kujenga uelewa wa pamoja

Naye Diwani wa Kata ya Haubi,Paulo Irovya,  ambapo zahanati hiyo, ipo alisema kwamba ataitisha Kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) ili kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizo onekana katika zahanati hiyo, hasa zilizo ndani ya uwezo wao badala ya kusubiria bajeti ya Halmashauri ambayo wakati mwingine haitoshi kutatua changamoto zote za jamii.

Katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mafai, Mursal Juma Doiyya, aliahidi  kuitisha mkutano wa kijiji na kuwahamasisha wanakijiji kujenga kichomea taka katika zahanati hiyo, sambamba na kuendeleza ujenzi wa nyumba ya wahudumu ambayo imeishia hatua ya lenta ambayo inauwezo wa kutumika na familia mbili. 

Vifaa vya Kisasa kwa ajili ya Huduma ya Mama na Mtoto vilivyowekwa katika zahanati hiyo, zikiwepo Mashine ya kuvuta uchafu puani kwa watoto waliozaliwa na matatizo na mashine ya oxygen zikiwa chini sakafuni, ndani ya chumba cha kujifungulia



Mashine maalum ya kuchemshia vifaa tiba, ikiwa chini sakafuni kwenye chumba cha kujifungulia



TGNP conducts a Gender-Responsive SAM Exercise in the Health Sector

 

• Health workers residing in Dispensary premises to be relocated

• Water challenge at the clinic highlighted

• Village leadership to oversee Dispensary waste incinerators

By Our Reporter, Kondoa; dejkt@gmail.com

Health workers at the Mafai Village Dispensary in Haubi Ward, Kondoa District Council, who were living in wards intended for maternal and child health services, have been instructed to find alternative housing to allow the wards to be utilized for their intended purpose.

SAM team during the visit to Mafai Dispensary 


Speaking in response to issues raised during the Gender-Responsive Social Accountability Monitoring (SAM) exercise conducted by the Tanzanian Gender Networking Programme (TGNP) in the health sector, the Acting Executive Director of the Kondoa District Council, Mashauri Visenti, stated that the health workers at the Mafai Dispensary, who were residing in the maternal and child health wards, should move to rented houses in the village to allow for efficient delivery of maternal and child health services in those rooms. This also ensures the safety of the equipment in the clinic.

"Since we have completed a year of operation for this Dispensary, we advise that those wards be vacated to further enhance the maternal and child health services in our clinic," said Mashauri.

Previously addressing this matter, the Health Secretary of the Kondoa District Council Lameck Mmaaga, mentioned that these workers were initially new and were deployed to establish the new Dispensary. They requested to reside in those rooms initially to become familiar with the environment and to find housing in the village.


Gender Responsive Social Accountability Monitoring (SAM) Facilitator; Mr. Deogratius Temba, conducted the Pre-SAM training for the team. 


"Now that they are acclimated to the environment and have spent over a year, initially we allowed this because they were establishing services in that village. We will write a letter to instruct them to find housing in the village so that the services can continue unobstructed. It's also not hygienic for health workers to live within the hospital or treatment rooms," stated Mmbaga.


SAM Traning was highly participatory

Presenting the SAM results to the Council stakeholders and Management, the SAM Facilitator from the Tanzanian Gender Networking Programme (TGNP), Deogratius Temba, noted that despite the budgetary challenges and the delivery of gender-sensitive health services, the Kondoa District Council had strived to allocate a gender-Responsive health budget, which also led to receiving a clean audit report according to the Controller and Auditor General's (CAG) report for 2021/2022.

Temba advised the Council to prioritize properly using and maintaining maternal and child health equipment. For instance, at the Mafai Dispensary, the maternal and child health wards are being used for accommodation, and the room that is currently serving as a ward and labor room is situated openly near the Outpatient Department (OPD). This lacks privacy for women in labor.

"Due to the non-use of the dedicated maternal and child health ward, the preservation and maintenance of maternal and child health equipment, as well as modern machines purchased for these purposes, are compromised. For instance, valuable machines like the Oxygen machine, newborn nasal suction machine, and modern sterilizer were found lying on the floor," Temba said, adding:

"We didn't observe any budget allocation for the Dispensary to ensure access to clean and safe water for the needs of delivering mothers. Even the nearby well at the Mafai Dispensary hasn't been utilized. Additionally, the women giving birth at the Dispensary lack access to water." Temba stated.


SAM team during the Analysis and Document review

Furthermore, the Gender-Responsive  SAM team recommended that the Council allocate a budget for staff housing, as there are half-built staff houses for health professionals that were constructed by the community but have been stalled for a long time. In the 2021/2022 fiscal year, no budget was allocated for rural health staff housing. For example, the staff house at the Mafai Dispensary, built by the community and has remained at the construction stage since 2014, is now deteriorating.

Oxygen machine and newborn nasal suction machine were found lying on the floor 



A modern sterilizer was found lying on the floor 

The Councilor of the Haubi Ward, Paulo Irovya, where the clinic is situated, pledged to convene a Ward Development Committee (WDC) meeting to devise strategies for addressing the challenges seen at the Dispensary, particularly those that are within their capacity, rather than solely relying on the Council's budget, which may not fully address all community challenges.

In the meeting, the Chairman of the Mafai Village, Mursal Juma Doiyya, promised to convene a village meeting and encourage villagers to construct waste incinerators at the clinic, as well as to continue the construction of staff houses, which have reached a construction phase suitable for housing two families.

Wednesday, August 9, 2023

UTPC yajengea uwezo wanahabari vinara wa jinsia

 Na Deogratius Temba, MOROGORO


UMOJA wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC),umejenga uwezo na kuunda timu ya Waandishi wa Habari vinara wa Jinsia (Gender Champions) watakaokuwa chachu ya kuongeza dhana ya uandishi wa Habari za Kijinsia nchini. 

Mkurugenzi Mtendaji, UTPC, Kenneth Simbaya, akifungua mafunzo hayo mjini Morogoro


Mafunzo kwa waandishi wa Habari Vinara wa Usawa wa Kijinsia yamefanyika kwa muda wa siku mbili kujenga uwezo Zaidi kwa washiriki namna ya kuandika habari zenye mrengo wa Kijinsia katika sekta mbalimbali kwa ufadhili wa Ubalozi wa Sweden.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi  Mtendaji wa (UTPC) Kenneth Simbaya,akifungua mafunzo hayo amesema lengo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari, namna ya kuripoti habari za jinsia, pamoja na kujifunza namna ya kuandika au kuibua habari za kijinsia ambazo zimekuwa haziandikwi mara nyingi ili kuchoechea maendeleo endelevu kwa jamii yote kwa ujumla. 

Afisa Programme, Kutoka UTPC, Bi. Hilda Kileo akizungumza 


"Hakuna Maendeleo bila usawa wa kijinsia, Nchi yetu inatekeleza malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) tunataka kuona wanahabari wakielimisha jamii itambue haya malengo vizuri, jamii itambue namna ya kuhusisha maendeleo na SDGs" alisema Simbaya.

Aidha, amewataka pia waandishi wa habari kujikita katika kuandika habari za jinsia (Specialize), pamoja na kuandika habari kina zaidi na zenye kuleta uwajibikaji, na kubadilisha mitazamo hasi ndani ya jamii juu ya usawa wa kijinsia.

Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden Nchini Tanzania, Bi. Nasieku Kisambu akizungumza


Naye Ofisa Program kutoka UTPC Hilda Kileo, amesema mafunzo hayo pia yamelenga kufanikisha malengo endelevu ya Maendeleo (SDGs) lengo namba 5 Usawa wa Kijinsia  na kuyahusisha na Mikakati na mipango ya ndani ya nchi kama dira ya maendeleo ya Taifa ya Miaka mitano (Vision 2025), Mpango wa maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP), Sera ya Taifa ya Jinsia na Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na watoto (MTAKUWWA). 

“… kama ilivyoainishwa katika lengo namba 5 la SDGs tunataka kuona wanahabari wa habari za Kijinsia wakiwa na uwezo wa kuunganisha utekelezaji wa mipango ya ndani ya nchi, huduma za Jamii na usawa wa Kijinsia. Lakini pia kutoa elimu kwa jamii ili itambue kuwa nchi yetu inatekelezaje SDGs zote 17 kwa mrengo wa kijinsia” alisema Hilda

Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada

Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Sweden Tanzania Nasieku Kisambu, amesema wamefadhili mafunzo hayo wakiamini kwamba vyombo vya habari zinauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ndani ya jamii kuhusu masuala mazima ya usawa wa kijinsia, na kuahidi kuendelea kushirikiana na UTPC  na wanahabari kuhakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa kaatika Nyanja zote.

Nao baadhi ya waandishi wa habari wamesema mafunzo hayo yamewaongezea uwezo katika kuandika habari za usawa wa kijinsia.


Mwezeshaji wa Mafunzo, Mtaalamu wa Masuala ya Usawa wa Kijinsia, Deogratius Temba, akitoa mada

Waandishi wa habari vinara wa Jinsia wataendelea kuwa chachu ya mabadiliko katika uandishi wa habari za kijinsia, wakilenga kutoa elimu kwa jamii kubadili mitazamo hasa mila na desturi zinazokuza mfumo kandamizi, kusukuma mabadiliko ya kisheria na kisera ili kuweka mazingira salama kwa wanawake, watoto na makundi mengine yaliyoko pembezoni