Saturday, March 9, 2024

TGNP yawapiga msasa viongozi wanawake Kondoa

 TGNP yawapiga msasa viongozi wanawake Kondoa


Na Mwandishi wetu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefanyamafunzo ya kujenga uwezo wa uongozi na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafsi za uongozi na maamuzi

Mafunzo hayo ambyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Mwanamke Ongoza  unaotekelezwa na  TGNP kwa kushirikiana na Taasisi ya Aga Khan Foundation na Serikali ya watu wa Canada, unaolenga kujenga uwezo kwa viongozi wanawake walioko madarakani ili kuboresha utendaji wao kwa manufaa ya jamii na kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi.

Pia mradi huu, unataka kuondoa vikwzo vinavyo wafanya wanawake waliopewa dhamana ya uongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kiuongozi ipasavyo, ambavyo ni pamoja na shughuli za huduma na matunzo kama vile utafutaji wa maji, shughuli za nyumbani, kuhudumia wagonjwa na utunzaji wa watoto ambazo zinaweza kufanywa na mtu mwingine kwenye familia, ikiwa ni sambamba na kubalisha mitazamo, mila na desturi na tamaduni zilizopitwa na wakati ambazo zinakwamisha wanawake kushiriki kwenye uongozi.

Kwa upande wake, Diwani wa Viti maalum Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Madina Fentu, alisema kwamba, mradi huu umemsaidia kwa kiasi kikubwa kupata uelewa wa mambo mengi lakini pia mume wake ameweza kushiriki moja ya semina ambazo alinufaika nazo.

“kwa kweli, ile warsha wa wenza wa viongozi wanawake imetusaidia sana, wenza wetu waliposhiriki, tumeona mabadiliko, pamoja na kwamba mimi mume wangu alikuwa akinisaidia awali, lakini aliongeza sana kunisaidia, hasa pale ninapokuwa na majukumu mengi ya kiuongozi na kushindwa kuhudumia familia” alisema Madina

Mapendekezo yaliyotoka kwenye warsha hiyo ni pamoja na Halmashauri zianzishe kanuni ya utaratibu wa kuwatangaza wanawake viongozi wa mfano wa kuigwa  na jamii na wapewe nafasi ya kuonekana ili kubadilisha mitazamo hasi kwa jamii kwamba wanawake hawezi kuwa viongozi wazuri.

Kutoa elimu ya kubadilisha mitazamo hasi kwa viongozi wa dini zote, wazee wa mila, wazee maarufu ili wawe mstari wa mbele katika kubadilisha mitazamo hasi, Kuweka kanuni kali za kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, Udhalilishaji wa kijinsia wakati wa chaguzi, sambamba na kuendelea kuwaelimisha wanaume ili kuwasaidia wenza wao ambao ni viongozi wa kisiasa katika majukumu ya kifamilia ili waweze kuhsiriki vizuri kwenye majukumu yao.

Viongozi wanawake walioshiriki mafunzo hayo ni Madiwani  wa Kata, madiwani wa viti maalum, Wenyeviti wa Vitongoji, wajumbe wa serikali za Vijiji, viongozi wa vyama vya siasa, na viongozi wataalamu ngazi ya jamii.  

 


















Tuesday, March 5, 2024

TGNP yawapiga msasa wadau na viongozi wanawake Dodoma

 TGNP yawapiga msasa wadau na viongozi wanawake Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Kondoa

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Imewajengea uwezo wadau mbalimbali kutoka kwenye mashirika, asasi na vikundi vya kijamii kuhusu namna ya kuongeza Ushiriki wa Wanawake ngazi za uongozi na maamuzi Halmashauri ya Wilaya Kondoa Mkoani Dodoma

Mafunzo haya yanatolewa katika Halmashauri za Wilaya ya Kondoa,Morogoro na Mtwara, kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa ‘’Mwanamke Ongoza-She Leads’’ unaotekelezwa na TGNP kwa ufadhili wa Agakhan Foundation na Serikali ya Watu wa Canada unaolenga kuwezesha wanawake viongozi walioko madarakani kutekeleza majukumu yao vizuri ya kiuongozi na kuongeza ushiriki Zaidi wa wanawake kwenye nafasi za uongozi na maamuzi.



Mafunzo hayo yamewanufaisha jumla ya washiriki 30 ambao ni viongozi wa vikundi vya Bodaboda, Dini, vikundi vya kijamii, asasi za kiraia, watu maarufu wenye ushawishi, ambao baada ya mafunzo hayo wataenda kutoa elimu kwenye vikundi vyao na kushawishi wanawake kushiriki kikamilifu kwenye nafasi za maamu.

Mwezeshaji mwenza kutoka TGNP, Ester Wiliam alisema kwamba warsha hiyo inalenga  kuongeza uelewa wa dhana za jinsia na uongozi,ubainishaji wa fursa zilizopo katika mifumo ya vyama na kwenye jamii ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi,

Ameongeza kwamba washiriki hao, wamejengewa uwezo kubainisha na kuchambua  mifumo kandamizi inayomzuia mwanamke kushiriki katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi. 

“Mafunzo haya yanaenda kuongeza nguvu kwenye Tapo, kwasababu hawa tuliowajengea uwezo wanatoka kwenye makundi mengi, taasisi ndogondogo zinazofanya kazi katika kata ya Haubi, ambapo wakienda kupeleka ujumbe tutakuwa tumewafikia watu wengi sana” alisema Esther

Kwa upande wake Anna Ambrose, Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Haubi, amesema kwamba, mafunzo hayo yanaenda kubadilisha mitazamo ya jamii katika uwezo wa wanawake kuwa viongozi, lakini pia kubadilisha baadhi ya mila na desturi zinazokwamisha wanawake kuwa viongozi katika jamii hiyo.