SALVATORY NTANDU, Shinyanga
Uwepo wa Vituo vya Taarifa na
Maarifa Katika Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga umetajwa kuwa kichocheo
muhimu katika ujenzi wa Vuguvugu na mabadiliko chanya kwenye jamii ambapo
katika Kijiji cha Miyuguyu, Kata ya Kiloleli, wilayani Kishapu wamefanikiwa kuhamasisha
wananchi kujenga nyumba mpya ya Mwalimu na matundu 12 ya vyoo katika Shule ya
Msingi Miyuguyu.
![]() |
| Mwezeshaji kutoka TGNP akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wanajamii wa Kijiji cha Miyuguyu wakati wa tathimini ya mafanikio ya Vituo vya Taarifa na Maarifa. |
Hayo yamebainishwa katika Kikao
cha Tathimini ya hali ya utendaji kazi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa katika
kata hiyo, ambapo Agness Kwilasa katibu wa kituo hicho, amesema mafanikio hayo
yamesababishwa na hamasa iliyotokana na Bunge la jamii lililoendeshwa na Kituo
hicho kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji katika kata hiyo.
Vituo vya Taarifa na Maarifa huanzishwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwenye ngazi ya Kata, baada ya kufanya uraghibishi ambao huwawezesha wananchi kutambua nafasi yao, kwa kuibua changamoto, kuzichambua na kuweka mikakati ya kuzitatua wakiwa wameshirikiana na viongozi wao ngazi ya kitongoji, kijiji, kata na Halmashauri. Aidha, Vituo hivi hushirikiana na viongozi wa serikali za Vijiji kuendesha Bunge la Jamii ambalo ni seheu ya kujenga mijadala namna ya kututua changamoto hizo.
![]() |
| Jengo la matundu 12 ya vyoo ambayo jamii ya kijiji cha Miyuguyu walishirikiana na viongozi na wadau wengine kuyajenga baada ya kujengewa uwezo na TGNP |
Katibu huyo wa Kituo, amesema kabla ya kuanzishwa kwa
kituo hicho mwitikio wa jamii kushiriki shughuli za maendeleo ulikuwa mdogo
lakini baada ya Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) kufanya uraghibishi na
kuwawezesha kuanzisha Kituo, baadaye kuendesha midahalo ya Bunge la jamii, wananchi walielekeza
mijadala kwenye uhaba wa miundombinu kwenye sekta za elimu na afya, ambapo
waliafikiana na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo kwa haraka ili
kuweka mazingira mazuri katika upatikanaji wa elimu.
“ wakati wa uraghibishi tuliziibua
changamoto zilizokuwa zinakikabili kata yetu ambapo wananchi waliazimia kujenga
nyumba ya mwalimu ambaye alikuwa anaishi katika moja ya Ofisi katika Shule ya
Msingi Miyuguyu kutokana na uhaba wa makazi ya walimu,”amesema Kwilasa.
Naye Hamis Mashauri Ofisa
Mtendaji wa kijiji hicho amesema tatizo la uhaba wa nyumba za walimu katika
shule ya Msingi Miyuguyu linasababisha walimu kushindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo ndio maana wanakijiji walihamasika na kuamua kujenga nyumba hiyo ili
kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi.
“Shule hii inawanafunzi 524,
madarasa sita, walimu wapo sita na nyumba za walimu zipo tatu mbili zizojengwa
na serikali na moja iliyojengwa na wananchi baada ya Bunge la Jamii, mwalimu wa
kike yupo mmoja tu na inauhaba wa walimu 11,”amesema Mashauri.
Kwa upande wake Getrude Missana
Mwalimu wa shule ya Msingi Miyuguyu amesema awali kabla ya kujengewa nyumba
hiyo alikuwa anaishi katika moja ya ofisi katika Shuleni hapo hali iliyokuwa
inamuwia vigumu kutekeleza majukumu yake hadi alipohamia katika nyumba
iliyojengwa na wakazi wa kijiji hicho.
![]() |
| Wazee wa Kijiji hicho wakiwa kwenye vikundi vya majadiliano wakati wa tathimini. |
“Tunaiomba serikali ituboreshe
mazingira ya kazi ikiwemo ujenzi wa Makazi ya walimu katika vituo vya kazi ili
kutimiza majukumu yetu ipasavyo,hapa mimi ni mwalimu wa kike peke yangu
niliyesalia wengi wakipangiwa wanaomba uhamisho kutokana na changamoto hizi,”amesema
Missana.
Diwani wa kata hiyo, Edward
Manyama, aliishukuru TGNP kwa kuwajengea uwezo wananchi wa kata hiyo na
kujitambua hasa kuwa na moyo wa kujitoa katika shughuli za maendeleo.
![]() |
| Nyumba iliyojengwa na wananchi ili kumtoa mwalimu asiendelee kuishi kwenye darasa la shule hiyo , ambapo alikuwa akiishi na kukosa uhuru wa kutekeleza wajibu wake kikamilifu |
Alisema kwamba, pamoja na
Halmashauri kuanza kutatua kero
mbalimbali zinazowakabili wakazi wa kijiji cha Miyuguyu na vijiji vingine
ikiwemo ya walimu ambapo kwa sasa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa walimu 11
na waliopo ni sita pekee, bado nguvu ya jamii katika kushiriki kwenye shughuli
za maendeleo inahitajika sana.
![]() |
| Nyumba iliyojengwa na wananchi ili kumtoa mwalimu asiendelee kuishi kwenye darasa la shule hiyo , ambapo alikuwa akiishi na kukosa uhuru wa kutekeleza wajibu wake kikamilifu |
“Ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kishapu imeahidi kuleta walimu wapya katika Shule ya Msingi
Miyuguyu,niwaombe wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwao ili waweze kutimiza
majumu ya kuwafundisha watoto wetu,”amesema Manyama.
Awali akizungumza wajumbe wa
Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya
Kiloleli kwenye Kijiji cha Miyuguyu Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba, alipongeza jitihada zizofanikisha kujengwa
kwa nyumba ya mwalimu ambaye awali alikuwa akiishi kwenye darasa mojawapo
shuleni hapo.
“TGNP inawajengea uwezo wananchi
kupitia vituo hivi ili waweze kuibua changamoto zinazowakabili na kuzipatia
suluhisho wenyewe kwa kushirikiana na viongozi wao, ujenzi wa nyumba hii na
matundu ya vyoo 12 ni kielelezo kwamba Wakazi wa kijiji cha Miyuguyu
wamebadilika na wameamua kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa pamoja,”amesema
Temba na kuongeza:
“ sio hii tu, wakazi wa Kata hii
kupitia Bunge la Jamii wamefanikiwa kujenga matundu 24 ya vyoo katika shule ya
msingi Kiloleli, ambapo choo cha awali cha wnaafunzi kilikuwa kimejaa kabisa na
kutitia, Bunge la Jamii lilipofanyika pale shuleni, kila mwanajamii alitakiwa
kuangalia kile choo na kupendekeza jambo la
Mwisho.







No comments:
Post a Comment